Sunday, July 1, 2012

MKURUGENZI WA CRDB AFUNGUA TAWI JIPYA TEGETA

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk Charles Kimei akikata utepe kuzindua tawi jipya la benki hiyo Tegeta jijini Dar es Salaam

WATOTO WAPEWA MATONE YA VITAMINI A

Mmoja wa watoto waliopelekwa kupimwa afya zao katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam wakipatiwa dawa ya vitamini A na Mganga Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Dk Gunini Kamba

WAZIRI WA NISHATI NA UMEME AZINDUA MTAMBO WA UMEME

Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo akiwa katika mtambo wa umeme unaotumia gesi asilia  Ubungo kabla ya kuuzindua

Saturday, June 30, 2012

GARI LA WAGONJWA LILILOMBEBA DK ULIMBOKA LIKIINGIA KATIKA UWANJA WA NDEGE

Gari la wagonjwa lililombeba Dk Ulimboka likiingia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam tayari kusafirishwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

WANAHARAKATI WAKIWA WAMESHIKA MABANGO YENYE UJUMBE MBALIMBALI KUMUAGA DK ULIMBOKA ANAYEPEKWA NJE YA NCHI KWA MATIBABU

Baadhi ya wanaharakati na madaktari wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa aina mbalimbali kumuaga Dokta Stephen Ulimboka ambaye alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Monday, June 25, 2012

ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA WAKIULINDAMWENGE MARA BAADA YA KUINGIA JIJINI DAR ES SALAAM

Askari kutoka jeshi la Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.Picha: Aron Msigwa - MAELEZO

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM APOKEA MWENGE

Mkuu wa mkoa wa Dar es  Salam Saidi Meck Sadik (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Tatu Saidi Mussa leo jijini Dar es Salaam . Mwenge wa Uhuru umewasili  jijini  Dar es Salaam ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba.

WAKIMBIZA WAKIELEKEA KUANZA MBIO HIZO WILAYANI TEMEKE


Wakimbiza Mwenge kitaifa wakiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Capt. Ernest Mwanossa (wa kwanza mbele)  wakianza safari kuelekea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Temeke leo jijini Dar es Salaam.

MWENGE WA UHURU WAINGIA DAR

Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadik kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo miradi 11 itafunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi.

AIRTEL NA SUPA 5

Ni Mzee wa Makamo hivi lakini alionesha umahiri wake mkubwa wa kuwachangamsha vilivyo sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza.Anaitwa Mzee Salum akikamua jukwaani jana kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza,wakati wa uzinduzi  wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.