Monday, April 30, 2012

WAETHIOPIA HOI BAADA YA MGOMO WA KULA GEREZANI

Muuguzi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma akimsaidia mmoja wa wakimbizi kutoka Ethiopia walioishiwa na nguvu baada ya kugoma kula katika gereza la mkoa na kukimbizwa hospitalini hapo. Waethiopia hao walikuwa wakishinikiza kurejeshwa kwao baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kutolewa kwa msamaha wa Rais.

Askari Magereza wakimsaidia mmoja wa raia wa Ethiopia ambaye aliishiwa nguvu kutokana na mgomo wa kula chakula gerezani wakidai kurejeshwa kwao. Waethiopia hao walifungwa mwaka mmoja na kutolewa kwa msamaha wa Rais.

Dafrosa Longa (43) mkazi wa Kijiji cha Lipinyapinya katika Mtaa wa
Kigamboni Peramiho mkoani Ruvuma akiwa amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho jana baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu kwenye sherehe ya Kipaimara katika Kijiji cha Namihoro, Peramiho Songea mkoani Ruvuma. (PICHA: FRIDAY SIMBAYA)
Rais Jakaya Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment