Monday, May 21, 2012
Mwanamitindo wa kimataifa mtanzania Flaviana Matata anayefanya kazi zake nchini Marekani akiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya pamoja ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya MV.Bukoba iliyotokea Mei 21 mwaka 1996 wakati meli hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka Bukoba kuelekea Mwanza. Mama mzazi wa Flaviana ni miongoni mwa abiria zaidi ya 1000 wanaokadiriwa kufariki katika ajali hiyo, ambapo mwanamitindo huyo alitumia kumbukumbu ya ajali hiyo iliyofanyika jana katika makaburi hayo eneo la Igoma Jijini Mwanza kutoa msaada wa makoti ya kujiokolea (life jackets) 500 kwa kampuni ya meli nchini (MSC) ambayo yatatumiwa na abiria kujiokolea endapo itatokea ajali nyingine. (Picha: George Ramadhan).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment