Wananchi wa Kata ya Madibila
wilayani Mbarali wakiangalia mashine mpya ya kuvunia mpunga iliyonunuliwa kwa
ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na Chama cha Wakulima wa Mpunga
(Mamcos) wakati ikifanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa rasmi. Mashine hiyo
ilinunuliwa kwa thamani ya shilingi milioni 66 kutoka kampuni ya Farm Equip
Tanzania Ltd ya Jijini Dar es Salaam na ilikabidhiwa juzi kwa wakulima hao.
No comments:
Post a Comment