Monday, May 21, 2012

FLAVIAN MATATA AKABIDHI MAJAKETI YA KUJIOKOLEA KATIKA KUMBUKUMBU YA MV BUKOBA

Mwanamitindo Flaviana Matata (kushoto) akivaa koti la kujiokolea (life jacket) kama ishara ya kukabidhi msaada wa jumla ya makoti 500 kwa Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza Elias Makory (kulia) aliyekuwa mgeni rasmi katika kumbukumbu ya ajali ya MV.Bukoba iliyofanyika jana katika makaburi ya pamoja ya watu waliokufa katika ajali hiyo yaliyopo Igoma JijiniMwanza.
Mama mzazi wa mwanamitindo huyo ni miongoni mwa watu zaidi ya 1000 wanaokadiriwa kuzama na kupoteza maisha katika ajali hiyo mbaya kabisa ya kwanza kutokea hapa nchini.(Picha:George Ramadhan)

No comments:

Post a Comment