Sunday, July 1, 2012
MKURUGENZI WA CRDB AFUNGUA TAWI JIPYA TEGETA
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk Charles Kimei akikata utepe kuzindua tawi jipya la benki hiyo Tegeta jijini Dar es Salaam
WATOTO WAPEWA MATONE YA VITAMINI A
Mmoja wa watoto waliopelekwa kupimwa afya zao katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam wakipatiwa dawa ya vitamini A na Mganga Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Dk Gunini Kamba
WAZIRI WA NISHATI NA UMEME AZINDUA MTAMBO WA UMEME
Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo akiwa katika mtambo wa umeme unaotumia gesi asilia Ubungo kabla ya kuuzindua
Saturday, June 30, 2012
GARI LA WAGONJWA LILILOMBEBA DK ULIMBOKA LIKIINGIA KATIKA UWANJA WA NDEGE
Gari la wagonjwa lililombeba Dk Ulimboka likiingia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kusafirishwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu.
WANAHARAKATI WAKIWA WAMESHIKA MABANGO YENYE UJUMBE MBALIMBALI KUMUAGA DK ULIMBOKA ANAYEPEKWA NJE YA NCHI KWA MATIBABU
Baadhi ya wanaharakati na madaktari wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa aina mbalimbali kumuaga Dokta Stephen Ulimboka ambaye alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Monday, June 25, 2012
ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA WAKIULINDAMWENGE MARA BAADA YA KUINGIA JIJINI DAR ES SALAAM
Askari kutoka jeshi la
Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo
jijini Dar es Salaam.Picha: Aron Msigwa -
MAELEZO
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM APOKEA MWENGE
Mkuu wa mkoa wa Dar
es Salam Saidi Meck Sadik (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa
mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Tatu Saidi Mussa leo jijini Dar es Salaam . Mwenge wa
Uhuru umewasili jijini Dar es Salaam
ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba.
WAKIMBIZA WAKIELEKEA KUANZA MBIO HIZO WILAYANI TEMEKE
Wakimbiza Mwenge
kitaifa wakiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Capt. Ernest Mwanossa (wa
kwanza mbele) wakianza safari kuelekea maeneo mbalimbali ya wilaya ya
Temeke leo jijini Dar es Salaam.
MWENGE WA UHURU WAINGIA DAR
Mkuu wa wilaya ya
Temeke Bi. Sophia Mjema akiahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi
Meck Sadik kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza katika maeneo mbalimbali ya
wilaya hiyo ambapo miradi 11 itafunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
AIRTEL NA SUPA 5
Ni Mzee wa Makamo hivi lakini alionesha umahiri wake mkubwa wa
kuwachangamsha vilivyo sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza.Anaitwa Mzee
Salum akikamua jukwaani jana kwenye viwanja vya Furahisha jijini
Mwanza,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5.
Sunday, June 24, 2012
EATV WAPAGAWISHA VIJANA KATIKA SHINDANO LA DANCE 100 LILILOFANYIKA TEMEKE
Wasanii wa kikosi cha T Africa kutoka Temeke wakicheza kuwania nafasi ya Tano Bora katika mashindano ya Dance 100 yaliyoandaliwa na EATV katika viwanja vya TCC,Chang;ombe jijini Dar es Salaam ambapo kundi litakaloshinda baada ya mpambano wa makundi kutoka Kinondoni,Ilala na Temeke atajinyakulia shilingi milioni 5
HAWA NDO BEST FRIEND
Wasanii wa kundi la BEST FRIEND wakicheza kutafuta nafasi ya
Tano Bora Temeke katika mashindano ya Dance 100 yaliyoandaliwa na EATV
katika uwanja wa TCC Club Chang;ombe jijini Dar es Salaam.
BEST FRIEND KIBKO WILAYNI TEMEKE
BEST FRIEND SI MCHEZO
Kundi la BEST FRIEND wakicheza kutafuta nafasi ya
Tano Bora Temeke katika mashindano ya Dance 100 yaliyoandaliwa na EATV
katika uwanja wa TCC Club Chang;ombe jijini Dar es Salaam.
WASANII WA KUNDI LA BEST FRIEND WANOGESHA MAMBO
Wasanii wa kundi la BEST FRIEND wakicheza kutafuta nafasi ya
Tano Bora Temeke katika mashindano ya Dance 100 yaliyoandaliwa na EATV
katika uwanja wa TCC Club Chang;ombe jijini Dar es Salaam.
WASANII WA BEST FRIEND WAKICHACHAFYA
WASANII WA KUNDI LA BEST FRIEND WATIA FORA
Wasanii wa kundi la BEST FRIEND wakicheza kutafuta nafasi ya
Tano Bora Temeke katika mashindano ya Dance 100 yaliyoandaliwa na EATV
katika uwanja wa TCC Club Chang;ombe jijini Dar es Salaam.
WASANII WA KIKUNDI CHA MIA KWA MIA
Wasanii maarufu kwa jina la Mia kwa Mia wakicheza kutafuta nafasi ya
Tano Bora Temeke katika mashindano ya Dance 100 yaliyoandaliwa na EATV
katika uwanja wa TCC Club Chang;ombe jijini Dar es Salaam.
Saturday, June 23, 2012
EATV WAPAGAWISHA VIJANA WA ILALA
Vijana wa kundi la Cool Jackson wakionyesha utaalam wao wa
kucheza katika hatua za awali za kutafuta vikundi vitano kutoka wilaya ya Ilala
ambavyo vitaingia katika kinyanganyiro cha kutafuta kundi bora ambalo
litajinyakulia zawadi ya shilingi milioni 5 kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Mashindano hayo yameandaliwa na kituo cha televisheni kwa vijana cha Channel 5.
Mashindano hayo yanaendelea leo kwa wilaya ya Temeke katika uwanja wa Sigara
Chang’ombe.
KUNDI LA FBI LAONYESHA UMAHIRI KWENYE MICHUANO WA DANCE 1000 YA EATV
Wasanii wa FBI ya Ilala wakinyesha utaalam wao katika mashindano ya DANCE 100 yaliyotayarishwa na EATV kwa wilaya za Ilala,Temeke na Kinondoni kutafuta kundi bora ambalo lijinyakulia shilingi milioni 5
KUNDI LA GOMS UNIT NALO LAONYESHA MAKALI YAKE
Wasanii wa kundi la Goms Unit wakionyesha utalaam wao kwenye mashindano ya Dance 100 katika viwanja vya Don Bosco
WAPENZI WA FBI WAKIPAGAWA
Wapenzi wa kundi la FBI wakifurahia kundi hilo baada ya kuonyesha makali yao katika viwanja vya Don Bosco
WAPENZI WA MUZIKI WA CHANNEL 5 WAPAGAWISHWA A
Wapenzi wa mashindano ya DANCE 100 yaliyotayarishwa na EATV wakifuhia moja ya vikundi vilivyoshiriki kutoka Ilala.
EATV YAPAGAWISHA VIJANA WA ILALA
Wasanii
wa kikundi cha FBI wakionyesha umahiri wao wa kucheza katika hatua za awali za
kutafuta vikundi vitano kutoka wilaya ya Ilala ambavyo vitaingia katika
kinyanganyiro cha kutafuta kundi bora ambalo litajinyakulia zawadi ya shilingi
milioni 5 kwa mkoa wa Dar es Salaam jana. Mashindano hayo yameandaliwa na kituo
cha televisheni kwa vijana cha Channel 5. Mashindano hayo yanaendelea leo kwa
wilaya ya Temeke katika uwanja wa Sigara Chang’ombe
Friday, June 22, 2012
KABURI LA KUMHIFADHI MPENDWA WILLY EDWARD LAANDALIWA
Vijana wakichimba jana kaburi atakamohifadhiwa milele aliyekuwa Mhariri
Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward nyumbani kwao
Molotonga, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti, Mara jana.
WAZIRI LUKUVI AKIMBEMBELEZA MBUNGE WA BUSEGA AIUNGE MKONO BAJETI
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (Sera na Uratibu wa bunge), William
Lukuvi (kulia) akicha chemba na mbunge wa Busega, Luhaga Mpina nje ya lango la
nyuma la ukumbi wa bunge mjini Dodoma jana. Mpina ndio mbunge pekee wa CCM,
aliyekataa kuiunga mkono bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 kwa madai kuwa
haikuwa ile waliyokubaliana baina ya kamati ya fedha ya bunge na serikali
Thursday, June 21, 2012
MAMBO YA KEKI
Akiwa furaha kubwa Bi. Fatuma Katanga
akimlimsha kipande cha Keki mumewe Bwana
Amani Mahanga(Kushoto)wakati wa hafla fupi ya siku ya
kuzaliwa kwake katika iliyofanyika nyumbani kwao huko Buza
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
hivi karibuni.
MAMBO YA BIRTH DAY
Bi Fatuma Katanga akiwasha mishumaa wakati wa sherehe ya
siku ya kuzaliwa kwake iliyofanyika nyumbani kwao huko Buza nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.Wengine Pichani ni mumewe Amani Mahanga(Kushoto) na Binti yao pekee Mosi aliyeandaa
hafla hiyo.
(Picha na Moshy Kiyungi)
Subscribe to:
Comments (Atom)
