MREMBO Noela Michael (19),
usiku wa kuamkia jana alifanikiwa kutwaa taji la Tabata 'Miss Tabata 2012
katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Da’ West Park
jijini Dar es Salaam.
Noela ambaye awali alibwagwa
katika kuwania taji la talent aliweza kuwafunika warembo wengine 18 waliokuwa
wanawania taji hilo
lililokuwa linashikiwa na Faiza Ally.
Noela alizawadiwa shilingi
500,000 na king’amuzi iliyolipiwa miezi sita iliyotolewa na Multichoice.
Nafasi ya pili katika
shindano hilo
ilikwenda kwa Diana Simon (20) aliyeshinda Sh 500,000 watatu ni Wilhemina
Mvungi (21) alizawadiwa Sh 350,000), wanne ni Phillos Lemi (19) na Suzzane
Deodatus (20) alishika nafasi ya tano.Wote wawili walizawadiwa Sh 200,000 kila
moja.
Warembo hao watano
wataiwakilisha Tabata katika mashindano ya Kanda ya Ilala yatakayofanyika
baadaye mwaka huu.
Warembo wengine waliofanikiwa
kuingia hatua ya 10 walikuwa ni Angel Kisanga (22), Khadija Nurdin (18), Haika
Joseph (18), Queen Issa (20) na Neema Saleh (18). Wote walizawadiwa Sh 100,000
kila moja.
Queen Issa alifanikiwa kutwaa
taji la mrembo mwenye kipaji cha kucheza huku Mercy Mlay akiteuliwa kuwa mrembo
aliyekuwa na nidhamu ya juu tangu kuanza kwa shindano hilo. Queen na Mercy kila moja alizawadiwa Sh
100,000.
Warembo awliyosalia walipata
kifuta jasho cha Sh 50,000 kila moja.
Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa bendi
ya Mashujaa, Mashauzi Classic iliyoko chini ya Isha Ramadhani Mfalme na Costa
Sibuka.
Shindano hilo iliandaliwa na
Keen Arts na Bob Entertainment na kudhaminiwa na Dodoma Wine, Redds, Integrated Communications, Fredito
Entertainment, Multichoice Tanzania, Screen Masters, Kitwe General Traders,
Step In Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady Pepeta.
No comments:
Post a Comment