Wednesday, June 6, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE ACHANGISHA SH BILIONI 3.2 KWENYE HARAMBEE YA MKAPA HIV/AIDS FOUNDATION

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bw. Deo Mwanyika, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Barrick Tanzania baada ya kuibuka mchangiaji mkubwa kwa kutoa dola za Kimarekani laki 5 kwa ajili ya kuchangia taasisi ya Mkapa Hiv/Aids Foundation Jumanne Juni 5, 2012 usiku katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu  wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa aliyeandaa hafla hiyo iliyoweza kukusanya shilingi bilioni 3.2 na kuvuka malengo ya harambee hiyo kwa asilimia sita

No comments:

Post a Comment