Thursday, May 31, 2012

MWANASIASA MASHUHURI MZEE MUSTAPHA SONGAMBELE ATIMIZA MIAKA 87

Alhaji Mustafa Songambele na mkewe Mwaya Kondo wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa waliofika katika sherehe fupi ya kutimiza miaka 87 ya kuzaliwa kwa mwanasiasa huyo mkongwe hapa nchini,

Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Alhaji Mustafa Songambele kulia akizima mshumaa wakati wa siku yake ya kuzaliwa (birthday0baada ya kufikisha umri wa miaka 87,kushoto ni mke wake Bi Mwaya Kondo
Mwaya Kondo kushoto,akimlisha kipande cha keki mumewe Alhaji Mustafa Songambele wakati wakusherehekea siku ya kuzaliwa ya Mwanasiasa huyo mkongwe hapa nchini ambapo ametimiza umri wa miaka 87.
Alhaji Mustafa Songambele na mkewe Bi Mwaya kondo wakipigana mabusu ikiwa ni ishara ya upendo wao baada ya Songambele kutimiza miaka 87 ya kuzaliwa.
Alhaji Mustafa Songambele akionesha upendo kwa mkewe mama Mwaya Konddo kwa kumlisha kipande cha keki wakati wa sherehe za miaka 87 ya kuzaliwa kwa Mzee Songambele iliyofanyika nyumbani kwake.
Afisa Elimu wa Shule za Msingi jijini Mbeya Aulelia Lwenza akibadjhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milion 5  kwa baadhi ya Walimu Wakuu ambao ulitolewa na bodi ya makandarasi  jana wakati wa uzinduzi  mkutano wa mwaka 2012 jana katika chuo cha sayansi na teknonolojia (MIST) jana picha na Hawa Mathais,Mbeya)

Tuesday, May 29, 2012

IDD SIMBA ATINGA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Mwenyekiti wa zamani wa Shirika la Usafiri  la UDA, Iddi Simba a kiwa katika   Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Simba  alifikishwa katika mahakama hayo  kwa  kufunguliwa  mashtaka manane  yanahusiana na tuhuma za rushwa
Mwenyekiti wa zamani wa Shirika la Usafiri  la UDA, Iddi Simba a kiwa katika   Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Simba  alifikishwa katika mahakama hayo  kwa  kufunguliwa  mashtaka manane  yanahusiana na tuhuma za rushwa. PICHA: MPIGAPICHA WETU
Askofu wa kanisa la TAG Kariakoo mjini Zanzibar, Dickson Kaganga, ambaye kanisa lake limechomwa moto, akizungumza kwenye kikao hicho ambacho viongozi wa madhehebu mbalimbali walihudhuria.
Picha na Martin Kabemba

MH ESHIMIWA ABOOD AKITEMBEZWA KATIKA KANISA LILILOCHOMWA MOTO

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed 
Akitembezwa na mwenyeji wao, Askofu Dickson Kaganga,
 kwenye kanisa la TAG la Kariakoo Zanzibar kuangalia uharibifu uliosababishwa na kuchomwa moto na watu wasiojulikana hivi karibuniPicha na Martin Kabemba
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Thabit Noman Jongo akiongea katika kikao hicho.
Picha na Martin Kabemba.

WAZIRI ABOOD ATEMBELEA KANISA LILILOCHOMWA MOTO ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini baada ya kutembelea kanisa la TAG la Kariakoo mjini Zanzibar lililochomwa moto juzi.Add caption

Monday, May 21, 2012

Mfanyabiashara Augustine Kisinja ambaye ameshinda uwakala bora Tanzania kwa kuwa muuzaji na msambazaji mzuri wa vinywaji vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akiendesha Bajaj yenye thamani ya sh. mil. 4.7 aliyozawadiwa na kampuni hiyo hivi karibuni mjini Makambako, Njombe. Pia Kisinja alizawadiwa gari aina ya Jac Canter lenye thamani ya sh. milioni 47.

JUKWAA LA KATIBA LAWASILISHA MACHAPISHO MBALIMBALI KWA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA

Waziri wa Katiba na Sheria  Bw. Mathias Chikawe akipokea  machapisho mbalimbali  kutoka kwa Bw. Hebron Mwakagenda wa  Kamati Ongozi ya Jukwaa la Katiba Tanzania wakati wajumbe wa Jukwaa hilo walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Mei 21, 2012). Wanaoshuhudia ni Bi. Ussu Mallya na Bw. William Kahale  kutoka Jukwaa hilo.    
Mwanamitindo wa kimataifa mtanzania Flaviana Matata anayefanya kazi zake nchini Marekani akiweka shada la maua katika moja ya makaburi ya pamoja ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya MV.Bukoba iliyotokea Mei 21 mwaka 1996 wakati meli hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka Bukoba kuelekea Mwanza. Mama mzazi wa Flaviana ni miongoni mwa abiria zaidi ya 1000 wanaokadiriwa kufariki katika ajali hiyo, ambapo mwanamitindo huyo alitumia kumbukumbu ya ajali hiyo iliyofanyika jana katika makaburi hayo eneo la Igoma Jijini Mwanza kutoa msaada wa makoti ya kujiokolea (life jackets) 500 kwa kampuni ya meli nchini (MSC) ambayo yatatumiwa na abiria kujiokolea endapo itatokea  ajali nyingine. (Picha: George Ramadhan).

FLAVIAN MATATA AKABIDHI MAJAKETI YA KUJIOKOLEA KATIKA KUMBUKUMBU YA MV BUKOBA

Mwanamitindo Flaviana Matata (kushoto) akivaa koti la kujiokolea (life jacket) kama ishara ya kukabidhi msaada wa jumla ya makoti 500 kwa Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza Elias Makory (kulia) aliyekuwa mgeni rasmi katika kumbukumbu ya ajali ya MV.Bukoba iliyofanyika jana katika makaburi ya pamoja ya watu waliokufa katika ajali hiyo yaliyopo Igoma JijiniMwanza.
Mama mzazi wa mwanamitindo huyo ni miongoni mwa watu zaidi ya 1000 wanaokadiriwa kuzama na kupoteza maisha katika ajali hiyo mbaya kabisa ya kwanza kutokea hapa nchini.(Picha:George Ramadhan)

Saturday, May 19, 2012

Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara cha Moshi mkoani Kilimanjaro,Prof Faustine Bee akizungumza katika hafla ya Siku ya Wanafunzi iliyofanyika chuoni hapo juzi mabpo mgeni rasmi alikuwa Dk. Reginald Mengi
Wanafuzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara wakimsikiliza Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi akiwahutubia

SIKU YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA USHIRIKA NA BIASHARA

Catherin Paul wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara akitoa mada katika Siku ya Wanafunzi iliyofanyika Chuoni hapo juzi ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Marekani Barrack Obama
Rais Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano wa Chakula unaofanyika nchini Marekani

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIZUNGUMZA KATIKA KITUO CHA CSIS-MAREKANI

Rais Jakaya Kikwete akizungumza kituo cha CSIS nchini Marekani

Friday, May 18, 2012

Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Simba Patrick Mafisango kwenye viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam leo
Sehemu ya umati wa watu waliokwenda kuuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Simba Patrick Mafisango katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam leo
Waombolezaji wakilia mara baada ya kuuona mwili wa marehemu Patrick mafisango aliyekuwa mchezaji wa Simba wakati wa kutoa heshima za mwisho 
Nahodha wa Simba Juma Kaseja akilia wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa mchzaji wa Simba Patrick mafisango katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam

HARUNA MOSHI AANGUA KILIO

Mchezaji wa Simba Haruna Moshi Boban akilia baada ya kuuona mwili wa aliyekuwa mchezaji mwenzake Patrick Mafisango wakati wa kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam
Mchezaji wa Simba Uhuru Selemani akilia wakati wa kutoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa Patrick Mafisango aliyekuwa mchezaji mwenzake. Mafisango alifariki kwa ajali ya gari ambapo alisafirishwa kwenda kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mazishi
Mwenyekiti wa Yanga Lyoid Nchunga akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Simba Patrick Mafisangoaliyeagwa katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam leo
Leonard Thadeo akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Patrick Mafisango akwenye viwanja vya Sigara leo

MWENYEKITI WA SIMBA AANGUA CHOZI

Add caption
Mwenyekiti wa Simba Ismail Adwen Rage akitulizwa na Prof Philemon Sarungi baada ya kiongozi huyo kushindwa kutoa salam za klabu yake na kuanza kulia katika viwanja vya Sigara ambako kulifanyika maombolezo ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo Patrick Mafisango aliyefariki kwa ajali ya gari juzi.

KWAHERI PATRICK MAFISANGO

Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Simba Patrick Mafisango likiwa limewekwa katika hema kwenye uwanja wa Sigara tayari kwa kuagwa na wapenzi wanamichezo leo

Wednesday, May 16, 2012

MINZIRO ACHARUKA KWA KUDAI MSHAHARA WAKE AMBAO HAJALIPWA

Kocha msaidizi wa Yanga Fred Felix Minziro asema kuwa naye anaudai uongozi mishahara ya miezi mitatu na pia posho mbalimbali ambazo yeye na wachezaji hawajalipwa. hayo ameyasema leo katika mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Travetine Magomeni jijini Dar es Salaam pia ametishia kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo

MKUU WA WILAYA YA BAHI BETTY MKWASA AWAUNGA MKONO WAUZA KARANGA

Mkuu wa wilaya ya bahi Betty Mkwasa akiwaunga mkono wakina mama wanaofanya biashara ndogondogo ya kuuza karanga mbichi mjini dodoma aliye simama ni bwana Juma Kengele  (Picha na Chris Mfinanga

RAIS ZANZIBAR AZUMGUMZA NA MAOFISA WA WIZARA YA BIASHARA NARais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashra,Viwanda na Masoko,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar jana. [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]VIWANDA

  1. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
  2. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashra,Viwanda na Masoko,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo Ikulu Mjini Zanzibar LEO.  [ Picha  na (,IKULU ZANZIBAR]
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi(wapili tola kushoto) akicheza mziki wa kwaito na Beaty Mkwasa Mkuu wa Wilaya ya Bahi (wa mwisho kulia)mara baada ya kumalizika kwa sherehe ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya Mkoani Dodoma leo

WAKUU WA WILAYA WA KONGWA NA KONDOA WAAPISHWA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema nchimbi (katikati) akifurahia jambo na Wakuu wa Wilaya  Kongwa Martha Umbulla (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Omary Kwaang’u
PICHA NA IBRAHIM  JOSEPH
Add caption

ASKARI KAMPUNI YA ULINZI WAGOMA MWANZA

Baadhi ya askari wa kampuni ya Ulinzi ya Victoria Support Services (VSS) wakiwa wamekusanyika katika ofisi za kampuni hiyo kushinikiza kulipwa mishahara yao ya miezi miwili iliyopita, ambapo pia walitishia kuchoma moto au kuvunja vioo vya magari ya kampuni hiyo endapo uongozi utashindwa kuwalipa haki yao hiyo (Picha: George Ramadhan)
Add caption

Tuesday, May 15, 2012

JIPE RAHA MWENYEWE

Mzee akiwa kwenye mapumziko baada ya kupata kinywaji kidogo baada ya saa za kazi huko mjini Singida

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KIKUNDI CHA WAFUGA NYUKI KUTOKA ZANZIBAR

Mheshimiwa Waziri mkuu Mizengo Pinda amekutana na kikundi kinacho jishughulisha na ufugaji nyuki kutoka pemba zanziba kikundi ambacho kinadhaminiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF  ambacho kilitembelea katika shamba la mh waziri mkuu lilipo eneo la ZUZU dodoma nakujionea jinsi ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa ziara hiyo ya mafunzo siku mbili imedhaminiwa na TASAF

Mizinga ya nyuki ya Waziri Mkuu

Hii ni mizinga ya nyuki ambayo inamilikiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni mfugaji mashuhuri wa nyuki. Picha na Christopha Mfinanga
Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakazi wa Tazara Makao Makuu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakazi wa Tazara Makao Makuu jijini Dar es Salaam

MWAKYEMBE AUNGURUMA TARAZA

Mmoja wa wafanyakazi wa Tazara akizungumza kwenye mkutano na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe wakati alipofanya ziara Makao Makuu jijini Dar es Salaam jana.

MAZOEZI YA KUOGELEA

Haya ni mazoezi maalum ya kuogelea ambapo vikundi mbalimbali vilishiriki katika kuogelea yaliyofanyika katika bwawa lililopo katika Shule ya kimataifa ya Hopac. Mashindano hayo yaliandaliwa na Chama cha Kuogelea.nchini.

HILI NI JANGUSHO LA NAZI KULE NG'APA MKOANI LINDI

Mkwezi akikusanya nazi alizoangusha ikiwa ni sehemu ya makusanyo ambayo tayari kwa kuwauzia wateja wakubwa ambao hununua kwa jumla katika kijiji cha Ng'apa mkoani Lindi
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaini katika kompyuta kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya 'Stand up for African women' inayoratibiwa na Shirika la Amref. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia zawadi ya saa aliyopewa na uongozi wa Amref yenye ujumbe wa 'stand up for African women' mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya kuchangia mafunzo ya wakunga ili kuokoa maisha ya mama na mtoto barani Africa yaliyofanyika Mnazi mmoja jijini Dar